Philippians 3:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mungu ataliweka wazi hilo nalo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sisi sote tuliokua kiroho tunapaswa kufikiri namna hii. Na ikiwa kuna jambo lolote ambalo hamkubaliani nalo, Mungu atalifunua kwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu ataliweka wazi hilo nalo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mwenyezi Mungu ataliweka wazi hilo nalo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mungu atawafunulia hilo nalo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, sote tulio watimilifu tuyafuate mawazo hayo! Kama liko, mwawazalo kuwa jinginejingine, hilo nalo Mungu atawafunulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi wote tunaokomaa kiroho, tukuwe na shabaha hiyo moja. Na kukiwa wamoja katikati yenu wanaokuwa na mafikiri mbalimbali, Mungu atawafunulia maneno yale.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo.