Philippians 3:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimekwisha waambieni jambo hili mara nyingi, na sasa narudia tena kwa machozi: Watu wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana, kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi, watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wapo wengi ambao mwenendo wao unaonesha kuwa ni adui za msalaba wa Kristo. Nimekwishawaambia kuhusu hao mara nyingi. Na inanifanya nitokwe machozi ninapowaambia kuhusu watu hao sasa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimekwisha waambieni jambo hili mara nyingi, na sasa narudia tena kwa machozi: Watu wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimekwisha waambieni jambo hili mara nyingi, na sasa narudia tena kwa machozi: watu wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana, kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi, watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana, kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi, watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wengi huenda, ambao nimewaambia mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimekwisha waambieni jambo hili mara nyingi, na sasa narudia tena kwa machozi: Watu wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wengi huendelea, kama nilivyowaambia mara nyingi, lakini sasa nawaambia kwa kuwalilia: Ndio wachukivu wa msalaba wake Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi nimewaambia mara nyingi, nami ninawaambia tena kwa machozi: kuna watu wengi wanaoonyesha kwa njia ya mwenendo wao kwamba kufa kwa Kristo juu ya musalaba ni chukizo kwao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana wengi huenenda, nimewaambieni marra nyingi khabari zao, na hatta sasa nawaambieni kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;