Philippians 3:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwisho wa watu hao ni maangamizi, mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu, na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanauendea uharibifu kwa namna wanavyoishi. Wanaabudu tamaa za mili yao kana kwamba hizo ndizo Mungu. Wanatenda mambo ya aibu na wanajivuna kwa kutenda mambo hayo. Wanayawazia mambo ya kidunia tu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwisho wa watu hao ni uangamivu, Mungu wao ni tumbo na utukufu wao ni aibu na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwisho wa watu hao ni maangamizi, mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu, na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao uko katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwisho wao ni kuangamia, mungu wao ni tumbo, utukufu wao umo katika mambo yenye soni, ndio wanaoyawaza tu yaliyopo nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwisho wao ni uharibifu, sababu mungu wao ni kushibisha tumbo zao. Wanajivuna kwa kufanya mambo ya kuwafezehesha. Nayo mafikiri yao ni juu ya vitu vya dunia hii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.