Philippians 3:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nilitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa kwangu; mimi ni wa taifa la Israeli, kabila la Benyamini, Mwebrania halisi. Kuhusu kuizingatia sheria mimi nilikuwa Mfarisayo,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania. Kwa habari ya Torati, ni Farisayo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa. Mimi ni Myahudi wa kabila la Benjamini. Mimi ni Mwebrania halisi, hata wazazi wangu pia. Nikawa Farisayo na nilitii torati kwa uangalifu sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi nilitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa kwangu; mimi ni wa taifa la Israeli, kabila la Benyamini, Mwebrania halisi. Kuhusu kuizingatia sheria mimi nilikuwa Mfarisayo,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mimi nilitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa kwangu; mimi ni wa taifa la Israeli, kabila la Benyamini, Mwebrania halisi. Kuhusu kuizingatia sheria mimi nilikuwa Mfarisayo,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania. Kwa habari ya sheria, ni Farisayo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania. Kwa habari ya sheria, ni Farisayo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari za kuishika torati, ni Farisayo,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nilitahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa kwangu; mimi ni wa taifa la Israeli, kabila la Benyamini, Mwebrania halisi. Kuhusu kuizingatia sheria mimi nilikuwa Mfarisayo,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nilitahiriwa siku ya nane ya kuzaliwa; kabila langu ni Mwisiraeli wa shina la Benyamini, ni Mwebureo mwenyewe, kwa chama cha Maonyo nalikuwa Fariseo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilitahiriwa nilipokuwa na umri wa siku nane. Mimi ni Mwisraeli, wa kabila la Benjamina, Mwebrania wa asili kabisa. Kuelekea mambo ya Sheria ya Kiyuda, nilikuwa Mufarisayo,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nalitabiriwa siku ya nane, ni lutu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamin, Mwebrania wa Waebrania, kwa khabari ya kuifuata sharia, Farisayo, kwa khabari ya wivu, mwenye kuliudhi Kanisa,