Philippians 4:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji langu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana Isa, ninyi wapendwa wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaka na dada zangu wapenzi, ninawapenda na ninataka kuwaona. Mnanifurahisha na ninajivuna kwa sababu yenu. Endeleeni kuwa imara kumfuata Bwana kama nilivyowaambia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana, ninyi wapenzi wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana Isa, ninyi wapenzi wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninawaonea shauku, furaha yangu, na taji langu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, ninaowatunukia, m furaha yangu na kilemba changu; wapenzi, simameni vivyo hivyo kwake Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo wandugu zangu wapendwa, niko na hamu sana ya kuwaona tena. Ninyi ndio munaokuwa furaha yangu na zawadi ya ushindi nitakayopokea. Ninyi wapendwa wangu, ninawaomba musimame imara katika ushirika wenu na Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.