Philippians 4:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nina furaha kubwa katika Bwana Isa kwamba hatimaye mmeanza upya kushughulika tena na maisha yangu. Kweli mmekuwa mkinifikiria lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kufanya hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimefurahi sana katika Bwana kwa sababu mmeonesha tena kuwa mnanijali. Mmeendelea kujali juu yangu, lakini haikuwepo njia ya kuonesha hili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nina furaha kubwa katika Bwana kwamba hatimaye mmeanza upya kushughulika tena na maisha yangu. Kweli mmekuwa mkinifikiria lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kufanya hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nina furaha kubwa katika Bwana Isa kwamba hatimaye mmeanza upya kushughulika tena na maisha yangu. Kweli mmekuwa mkinifikiria lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kufanya hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo, nilivyo mwake Bwana, nalifurahi sana, ya kuwa siku hizi mmekwisha pata tena kunitunza mimi. Tangu kale mlikuwa mkiyawaza, lakini siku za kati hamkuweza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipata furaha kubwa katika kuungana na Bwana kwa kuona munakumbuka tena kunisaidia. Sitaki kusema kwamba mulinisahau, lakini hamukupata wakati wa kuonyesha kwamba munanishugulikia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha fikara zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu; lakini hamkupata nafasi.