Philippians 4:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naam, nakusihi wewe pia, mwenzangu mwaminifu, uwasaidie hawa wanawake, kwa sababu walijitaabisha katika kazi ya Injili pamoja nami bega kwa bega, wakiwa pamoja na Klementi na watendakazi wenzangu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa ajili ya hili ninamwomba rafiki yangu aliyetumika pamoja nami kwa uaminifu: Wasaidieni wanawake hawa. Waliwahubiri watu Habari Njema kwa bidii kama watendaji wenzangu tukiwa pamoja na Klementi na wengine waliofanya kazi pamoja nami. Majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naam, nawasihi ninyi pia, wenzi wangu waaminifu, wasaidieni hawa wanawake, kwa sababu walijitaabisha katika kazi ya Injili pamoja nami bega kwa bega, wakiwa pamoja na Klementi na watenda kazi wenzangu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naam, nakusihi wewe pia, mwenzangu mwaminifu, uwasaidie hawa wanawake, kwa sababu walijitaabisha katika kazi ya Injili pamoja nami bega kwa bega, wakiwa pamoja na Klementi na watendakazi wenzangu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, nataka na wewe pia, mtumwa mwenzangu wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliofanya kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe, mwenzangu wa kweli, nakuomba, uwasaidie wanawake hao, maana waliupigania Utume mwema pamoja nami na pamoja na Klemensi nao wenzangu wengine wa kazi walioandikiwa majina yao katika kitabu cha uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wewe vilevile mutumishi mwenzangu mwaminifu, ninakuomba uwasaidie wanawake hao, kwa maana walisumbuka sana pamoja nami katika kazi ya kutangaza Habari Njema. Kuko vilevile Klementi na wenzangu wengine wa kazi. Hao wote majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.