Proverbs 11:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu anapoangamia, kuna shangwe za furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi, mwovu atowekapo, huwa kuna kelele za furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waongofu wakipata mema, mji huwashangilia, lakini wasiomcha Mungu wakiangamia, watu huwazomea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa haki wakipata fanaka, muji unashangilia. Waovu wakiangamia, watu wanapiga vigelegele.