Proverbs 11:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anayemdhamini mgeni atakuja juta, lakini anayechukia mambo ya dhamana yu salama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anayemdhamini mgeni atakuja juta, lakini anayechukia mambo ya dhamana yu salama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali ye yote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yuko salama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anayemdhamini mgeni atakuja juta, lakini anayechukia mambo ya dhamana yu salama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliyejitoa kuwa dhamana ya mgeni atapatwa na mabaya zaidi, lakini akataaye kumpa mwingine mkono hukaa na kutulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anayejitoa kulipia mugeni deni yake atajuta, lakini anayechukia mapatano yale ana usalama.