Proverbs 13:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu; wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu; wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana kitu cho chote mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuna mtu anayejitajirisha, lakini hana kitu; Kuna anayejifanya kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu; wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako wanaojitendekeza kuwa wenye mali, lakini hawana kitu, tena wako wanaojitendekeza kuwa maskini, lakini wana mali nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuna mutu anayejidai kuwa tajiri, kumbe hana kitu. Mwengine anajiona kuwa masikini wakati ana mali tele.