Proverbs 17:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi, na msema uongo hupatwa na maafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi, na msema uongo hupatwa na maafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huangukia kwenye taabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotovu huanguka katika misiba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi, na msema uongo hupatwa na maafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye moyo mdanganyifu hapati mema, naye mwenye ulimi wa upotovu huangushwa na mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwenye moyo mupotovu hafanikiwi, na musema uongo anapatwa na hasara.