Proverbs 17:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali Mwenyezi Mungu huujaribu moyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kalibuni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Bali Bwana huijaribu mioyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali BWANA huujaribu moyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali bwana huujaribu moyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Chungu cha kuyeyushia hujaribu fedha, nayo tanuru hujaribu dhahabu, lakini aijaribuye mioyo ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kalibuni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zahabu na feza vinapimwa kwa moto, lakini Yawe ndiye anayepima mioyo ya watu.