Proverbs 19:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mvivu ni kama mtu atiaye mkono katika sahani ya chakula, lakini hana nguvu ya kuuinua hadi mdomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mvivu ni kama mtu atiaye mkono katika sahani ya chakula, lakini hana nguvu ya kuuinua hadi mdomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mvivu huuzamisha mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuurudisha kwenye kinywa chake!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mvivu hutia mkono wake katika sahani; Wala hataki hata kuupeleka kinywani pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mvivu ni kama mtu atiaye mkono katika sahani ya chakula, lakini hana nguvu ya kuuinua hadi mdomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mvivu akiutia mkono wake katika bakuli haurudishi kinywani mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muvivu anatia mukono wake katika sahani lakini hauinui mpaka kwenye midomo.