Proverbs 29:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake kitakuwa thabiti daima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akataye mashauri ya wanyonge kwa kweli, kiti chake cha kifalme kitashupaa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme anayewaamua wamasikini kwa haki, ataona utawala wake unaimarika milele.