Proverbs 3:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa Mwenyezi Mungu humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa Bwana, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa BWANA humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa bwana humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mpotovu humtapisha Bwana, lakini wanyokao ndio, ambao anakula njama nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana waovu ni chukizo kwa Yawe, yeye anawafanya watu wa usawa kuwa warafiki zake.