Psalms 10:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
huotea mafichoni mwake kama simba. Huvizia apate kuwakamata maskini; huwanasa kwa mtego wake na kuwachukua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Akimkokota wavuni mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
huotea mafichoni mwake kama simba. Huvizia apate kuwakamata maskini; huwanasa kwa mtego wake na kuwachukua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
huotea mafichoni mwake kama simba. Huvizia apate kuwakamata maskini; huwanasa kwa mtego wake na kuwachukua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hunyata na kujifichaficha kama simba kichakani, humnyatia mnyonge, amkamate, humkamata mnyonge kweli na kumnasa tanzini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Akimkokota wavuni mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
anajificha katika maficho yake kama simba. Anavizia apate kuwakamata wamasikini; anawanasa kwa mutego wake na kuwachukua.