Psalms 104:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu mno! Umejivika utukufu na fahari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu. Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Wewe, Bwana, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu mno! Umejivika utukufu na fahari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Ee BWANA Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee nafsi yangu, umhimidi bwana. Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na utukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu mno! Umejivika utukufu na fahari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtukuze Bwana, roho yangu! Bwana Mungu wangu, u mkuu kabisa, yenye urembo na utukufu umeyavaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umusifu Yawe, ee nafsi yangu! Ee Yawe, Mungu wangu, wewe ni mukubwa kabisa! Umevaa utukufu na mamlaka.