Psalms 104:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha; naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miti ya Mwenyezi Mungu inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miti ya Bwana nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha; naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miti ya BWANA inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miti ya bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miti ya BWANA nayo imetoshelezwa maji, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha; naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata miti ya Bwana hunywa, mpaka ishibe, kama miangati ya Libanoni, aliyoipanda yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miti ya BWANA nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Miti mikubwa ya Yawe inapata maji ya kutosha; ndiyo mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.