Psalms 106:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazee wetu walipokuwa Misri, hawakujali matendo ya ajabu ya Mungu; hawakukumbuka wingi wa fadhili zake, bali walimwasi kando ya bahari ya Shamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, ile Bahari ya Shamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazee wetu walipokuwa Misri, hawakujali matendo ya ajabu ya Mungu; hawakukumbuka wingi wa fadhili zake, bali walimwasi kando ya bahari ya Shamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baba zetu katika Misri Hawakuzingatia matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, Bahari ya Shamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazee wetu walipokuwa Misri, hawakujali matendo ya ajabu ya Mungu; hawakukumbuka wingi wa fadhili zake, bali walimwasi kando ya bahari ya Shamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baba zetu walipokuwako kule Misri, walipoyaona mataajabu yako hawakuerevuka, hawakuyakumbuka yale mema mengi, uliyawagawia, wakakataa kukutii kule baharini, kwenye Bahari Nyekundu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Babu zetu walipokuwa Misri, hawakujali matendo ya ajabu ya Mungu; hawakukumbuka wingi wa wema wake, lakini walimwasi kando ya bahari Nyekundu.