Psalms 110:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Zaburi ya Daudi) Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu: “Keti upande wangu wa kulia, hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu: “Keti upande wangu wa kulia, hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Zaburi Ya Daudi) BWANA amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kuume, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu: “Keti upande wangu wa kulia, hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu, mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaburi ya Daudi. Yawe anamwambia bwana wangu: “Ikaa na mamlaka kwa kuume kwangu mpaka nitakapowaweka waadui zako chini ya miguu yako.”