Psalms 111:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote, nikijumuika na jamii ya watu waadilifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msifuni Mwenyezi Mungu. Nitamtukuza Mwenyezi Mungu kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haleluya
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote, nikijumuika na jamii ya watu waadilifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msifuni BWANA. Nitamtukuza BWANA kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msifuni bwana. Nitamtukuza bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote, nikijumuika na jamii ya watu waadilifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haleluya! *Namshukuru Bwana kwa moyo wote kwenye mkutano wao wanyokao mioyo nako kwao wateule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haleluia! Nitamushukuru Yawe kwa moyo wangu wote, katika mukutano wa watu wa usawa.