Psalms 12:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi, safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri, naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maneno ya Mwenyezi Mungu ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi, safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri, naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maneno ya BWANA ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maneno ya bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi, safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri, naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maneno ya Bwana ndiyo maneno yaliyo mang'avu hufanana na fedha zilizoyeyushwa chunguni huku nchini, zilizong'azwa hivyo mara saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe anasema: “Kwa sababu wamasikini wanaugua, na wakosefu wanalia, sasa ninasimama, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.”