Psalms 123:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Wimbo wa Kwenda Juu) Nakutazamia kwa hamu, ee Mwenyezi-Mungu, nakuangalia wewe utawalaye huko juu mbinguni!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakutazamia kwa hamu, ee Mwenyezi-Mungu, nakuangalia wewe utawalaye huko juu mbinguni!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Wimbo Wa Kwenda Juu) Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti cha enzi kiko mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakutazamia kwa hamu, ee Mwenyezi-Mungu, nakuangalia wewe utawalaye huko juu mbinguni!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimeyainua macho yangu na kuyaelekeza kwako, ukaaye mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wimbo wa safari za kidini. Ninainua macho kwako, ee Yawe, wewe unayeikaa huko juu mbinguni!