Psalms 123:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama watumishi wamtegemeavyo bwana wao, kama mjakazi amtegemeavyo bibi yake, ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mpaka hapo utakapotuonea huruma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mjakazi yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hadi atakapotuhurumia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama watumishi wamtegemeavyo bwana wao, kama mjakazi amtegemeavyo bibi yake, ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mpaka hapo utakapotuonea huruma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo BWANA Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo bwana Mwenyezi Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama vile macho ya watumishi Yanavyoutegemea mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Yanavyoutegemea mkono wa bibi yake; Ndivyo macho yetu yanavyomtegemea BWANA, Mungu wetu, Hadi atakapoturehemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama watumishi wamtegemeavyo bwana wao, kama mjakazi amtegemeavyo bibi yake, ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mpaka hapo utakapotuonea huruma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama macho ya watumishi yanavyoitazama mikono ya bwana zao, au kama macho ya mjakazi yanavyoitazama mikono ya bibi yake, hivyo macho yetu humtazama Bwana Mungu wetu, hata atuhurumie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama watumishi wanavyomutegemea bwana wao, kama mujakazi anavyomutegemea bibi mukubwa wake, ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe, ee Yawe, Mungu wetu, mpaka hapo utakapotuonea huruma.