Psalms 131:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi) Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi; mimi si mtu wa majivuno. Sijishughulishi na mambo makuu, au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi; mimi si mtu wa majivuno. Sijishughulishi na mambo makuu, au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi.) Moyo wangu hauna kiburi, Ee BWANA, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Moyo wangu hauna kiburi, Ee bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi; mimi si mtu wa majivuno. Sijishughulishi na mambo makuu, au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana, moyo wangu haujikuzi, wala macho yangu hayatazami juu, wala sifuatii makuu na mataajabu yanishindayo nguvu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wimbo wa safari za kidini: wa Daudi. Ee Yawe, sina moyo wa majivuno; wala macho yangu si ya kiburi. Sijishugulishi na mambo makubwa, yale yanayokuwa ya ajabu sana kwangu.