Psalms 133:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni kama umande wa mlima Hermoni, uangukao juu ya vilima vya Siyoni! Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake, kuwapa uhai usio na mwisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni kama umande wa Hermoni ukianguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake, naam, uzima hata milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni kama umande wa mlima Hermoni, uangukao juu ya vilima vya Siyoni! Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake, kuwapa uhai usio na mwisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko bwana alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni kama umande wa mlima Hermoni, uangukao juu ya vilima vya Siyoni! Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake, kuwapa uhai usio na mwisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au ni kama umande ulioko Hermoni, nako kwenye milima ya Sioni unakufika. Kwani Bwana alikoagizia mbaraka, ndiko huko, kuwa kwenye uzima kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kama umande wa mulima Hermoni, unaoanguka juu ya vilima vya Sayuni! Kutoka huko Yawe anatoa baraka, ndio uzima wa milele.