Psalms 138:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninasujudu kuelekea hekalu lako takatifu; nalisifu jina lako, kwa sababu ya fadhili zako na uaminifu wako; kwa sababu umeweka jina lako na neno lako juu ya kila kitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa maana umeitukuza ahadi yako zaidi ya jina lako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninasujudu kuelekea hekalu lako takatifu; nalisifu jina lako, kwa sababu ya fadhili zako na uaminifu wako; kwa sababu umeweka jina lako na neno lako juu ya kila kitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, na jina lako juu ya vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninasujudu kuelekea hekalu lako takatifu; nalisifu jina lako, kwa sababu ya fadhili zako na uaminifu wako; kwa sababu umeweka jina lako na neno lako juu ya kila kitu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Penya Nyumba yako takatifu nitakutambikia, nalo Jina lako nitalishukuru kwa ajili ya upole wako na kwa ajili ya welekevu wako, kwani umelikuza Jina lako kwa kufanya mambo yapitayo yote, uliyoyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninainama uso mpaka chini kuelekea hekalu lako takatifu. Ninalisifu jina lako, kwa sababu ya wema na uaminifu wako. Umeheshimisha jina lako na neno lako kuliko vitu vyote.