Psalms 139:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwa hata moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwapo hata moja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwepo hata moja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipokuwa mimba tumboni mwa mama, macho yako yaliniona, nazo siku zangu zote zilikuwa zimeandikwa kitabuni mwako hapo, zilipoambiwa, zitokee; ilikuwa hapo, hata moja yao ilipokuwa haijawa bado.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe uliniona hata mbele sijazaliwa. Uliandika kila kitu katika kitabu chako; siku zangu zote ulizipanga, hata mbele hakujakuwa ile ya kwanza.