Psalms 14:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi) Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Mahalathi. Zaburi Ya Daudi) Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna atendaye mema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpumbavu husema moyoni mwake: Hakuna Mungu. Hawafai kitu, mapotovu yao hutapisha, anayefanya mema hayuko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi. Mupumbafu anajisemesha hivi katika moyo: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, matendo yao ni ya kuchukiza; hakuna hata mumoja anayetenda mazuri!