Psalms 144:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wavulana wetu wakue kikamilifu kama mimea bustanini; binti zetu wawe kama nguzo zilizochongwa kupambia ikulu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kurembesha jumba la kifalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wavulana wetu wakue kikamilifu kama mimea bustanini; binti zetu wawe kama nguzo zilizochongwa kupambia ikulu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kuremba jumba la kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kurembesha jumba la kifalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wavulana wetu wakiwa ujanani wawe kama miche Iliyostawi kikamilifu. Binti zetu wawe kama nguzo za pembeni Zilizochongwa ili kupamba nyumba ya mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wavulana wetu wakue kikamilifu kama mimea bustanini; binti zetu wawe kama nguzo zilizochongwa kupambia ikulu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wetu wa kiume katika ujana wao tunawaombea, wakue kama miti ya kupandwa iliyotunzwa vizuri! Nao wana wetu wa kike na wawe kama nguzo zilizochorwa vizuri kuwa mapambo yao majumba matukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika ujana wao, wana wetu wakuwe kama mimea iliyostawi vizuri; nao wabinti wetu wakuwe wazuri kama nguzo zilizochongwa kwa kupamba nyumba ya kifalme.