Psalms 16:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu watakatifu walio duniani, hao ndio wenye fahari, na ninapendezwa nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watakatifu waliopo katika nchi nimewaambia: Hawa ndio wakuu wa kweli, ndio wanipendezao kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na juu ya waaminifu katika inchi, ninaheshimu nguvu zao.