Psalms 17:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe mikononi mwa watu hao, watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. Uwajaze adhabu uliyowawekea, wapate ya kuwatosha na watoto wao, wawaachie hata na wajukuu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, mkono wako uniokoe na watu kama hawa, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe mikononi mwa watu hao, watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. Uwajaze adhabu uliyowawekea, wapate ya kuwatosha na watoto wao, wawaachie hata na wajukuu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe mikononi mwa watu hao, watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. Uwajaze adhabu uliyowawekea, wapate ya kuwatosha na watoto wao, wawaachie hata na wajukuu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkono wako, Bwana, uniokoe mikononi mwa waume, ambao kiume chao ni cha dunia hii, fungu lao nalo liko nchini tu. Matumbo yao uyajaze mali zako, washibe pamoja na wana wao, tena watakazozisaza waziachie hao watoto wao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, mukono wako uwafukuze kati ya watu, tukio lao likuwe kutengana na wanaokuwa wazima. Uwashibishe kwa akiba uliyowawekea, watoto wao nao washibe na kuacha sehemu, wawaachie hata na wajukuu wao.