Psalms 18:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alijifunika giza pande zote, mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka: mawingu meusi ya mvua ya angani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alijifunika giza pande zote, mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, chandarua chake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua angani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua ya angani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Akiwa katika giza la mawingu mazito yaliyojaa maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alijifunika giza pande zote, mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatumia giza kuwa ficho lake, limfunike pande zote likiwa kao lake; ndio mawingu meusi yenye mvua kali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipanda juu ya kerubi na kuruka, akaruka juu ya mabawa ya upepo.