Psalms 18:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulipowakemea maadui zako ee Mwenyezi-Mungu, ulipowatisha kwa ghadhabu yako, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Mwenyezi Mungu, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee Bwana, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulipowakemea maadui zako ee Mwenyezi-Mungu, ulipowatisha kwa ghadhabu yako, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako, sakafu ya bahari ikaonekana, misingi ya dunia ikawa wazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee BWANA, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulipowakemea maadui zako ee Mwenyezi-Mungu, ulipowatisha kwa ghadhabu yako, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, ilipoonekana mikondo ya maji, nayo misingi ya nchi ikafunuliwa kwa nguvu ya makaripio ya kwako, Bwana, na kwa ukali wa pumzi ya pua yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee BWANA, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwapiga waadui mishale yake, akawatawanya; alirusha umeme mukali, akawakimbiza.