Psalms 18:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alinyosha mkono kutoka juu akanichukua, kutoka katika maji mengi alininyanyua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kilindini cha maji makuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alinyosha mkono kutoka juu akanichukua, kutoka katika maji mengi alininyanyua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akanyosha mkono wake kutoka juu, akanishika, akanitoa kutoka katika maji mengi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alinishukia kutoka juu, akanichukua, Na kunitoa katika maji mengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alinyosha mkono kutoka juu akanichukua, kutoka katika maji mengi alininyanyua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akakunjua mkono toka juu, akanikamata, mle mlimo na maji mengi akanichopoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, ulipovikaripia, pumzi ya pua yako ilifunua vilindi vya bahari na misingi ya dunia ikaonekana.