Psalms 18:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu; Mungu wangu ni mwamba wangu, ninayemkimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ni ngome yangu na boma langu, tena ni mponya wangu, ni Mungu aliye mwamba wangu, kwa hiyo ninamjetea; ni ngao yangu na pembe ya kunipatia wokovu, tena ni kingo langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakupenda, ee Yawe, nguvu yangu!