Psalms 18:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninamwita Mwenyezi Mungu anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninamwita BWANA anayestahili kusifiwa, nami nimeokoka kutoka kwa adui zangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninamwita bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Namwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana atukuzwaye ndiye, ninayemwitia; ndipo, ninapookolewa mikononi mwao walio adui zangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe ni kikingio changu, kimbilio langu, mukombozi wangu, Mungu wangu, yule ambaye ninamukimbilia, ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu, munara wangu.