Psalms 18:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umenipa ngao yako ya kuniokoa; mkono wako wa kulia umenitegemeza; wema wako umenifanikisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hufanya msaada wa wokovu wako kuwa ngao yangu, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza; msaada wako umeniinua niwe mkuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umenipa ngao yako ya kuniokoa; mkono wako wa kulia umenitegemeza; wema wako umenifanikisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hunipa ngao yako ya ushindi, mkono wako wa kuume hunitegemeza, huinama chini ili kuniinua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umenipa ngao yako ya kuniokoa; mkono wako wa kulia umenitegemeza; wema wako umenifanikisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hunipa ngao ya kuniokoa, kuumeni kwako hunishikiza, napo hapo, unaponinyenyekeza, hunikuza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ananifundisha kupigana vita, mikono yangu iweze kuvuta upinde wa chuma.