Psalms 18:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita; uliwaporomosha maadui chini yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia chini yangu walioniondokea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita; uliwaporomosha maadui chini yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita, adui zangu uliwafanya wasujudu miguuni pangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe umenipa nguvu za vita, Hunitiishia chini yangu walionishambulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita; uliwaporomosha maadui chini yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hunivika nguvu ya kupiga vita, huwalaza chini yangu wao waniinukiao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia chini yangu walioniondokea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwaangamiza, wasiweze kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu.