Psalms 20:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua, atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni; kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa nafahamu kuwa Mwenyezi Mungu humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua, atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni; kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa nafahamu kuwa BWANA humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa nafahamu kuwa bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake; Atamjibu toka mbingu zake takatifu, Kwa matendo makuu ya wokovu Ya mkono wake wa kulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua, atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni; kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nimejua, ya kuwa Bwana humwokoa, aliyempaka mafuta; akamwitikia mbinguni palipo Patakatifu pake, akamtolea nguvu za kuumeni kwake ziokoazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake; Atamjibu toka mbingu zake takatifu, Kwa matendo makuu ya wokovu Ya mkono wake wa kuume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutainua bendera kwa kutukuza jina la Mungu wetu. Yawe akutimizie mapenzi yako yote!