Psalms 21:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji la dhahabu safi kichwani pake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani umemjia na kumletea magawio mema, nacho kichwa chake umekivika kilemba kilicho dhahabu tupu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umemutimizia mapenzi ya moyo wake; wala haukumukatalia ombi lake.