Psalms 21:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto. Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake, moto utawateketeza kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati utajitokeza, utawafanya kama tanuru la moto. Katika ghadhabu yake Mwenyezi Mungu atawameza, moto wake utawateketeza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto. Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake, moto utawateketeza kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake BWANA atawameza, moto wake utawateketeza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake bwana atawameza, moto wake utawateketeza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawateketeza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto. Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake, moto utawateketeza kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utawafanya kuwa kama jiko la moto, utakapowatokea, Bwana atawameza kwa makali yake, nao moto utawala.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukono wako, ewe mufalme, utawakamata waadui zako wote; mukono wako wa nguvu utawakamata wanaokuchukia.