Psalms 22:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi mnaomcha Mwenyezi-Mungu, msifuni! Mtukuzeni enyi wazawa wote wa Yakobo! Mcheni Mungu enyi wazawa wote wa Israeli!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi ambao mnamcha Mwenyezi Mungu, msifuni! Ninyi nyote wazao wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wa Israeli!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi mnaomcha Mwenyezi-Mungu, msifuni! Mtukuzeni enyi wazawa wote wa Yakobo! Mcheni Mungu enyi wazawa wote wa Israeli!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi ambao mnamcha BWANA msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi ambao mnamcha bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wana wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazawa wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi mnaomcha Mwenyezi-Mungu, msifuni! Mtukuzeni enyi wazawa wote wa Yakobo! Mcheni Mungu enyi wazawa wote wa Israeli!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi mmwogopao Bwana, mkuzeni! Vizazi vyote vya Yakobo na vimtukuze! Vizazi vyote vya Isiraeli na vimwangukie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaelezea wandugu zangu matendo yako; nitakusifu kati ya kusanyiko lao, nikisema: