Psalms 22:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana yeye hapuuzi au kudharau unyonge wa mnyonge; wala hajifichi mbali naye, ila humsikia anapomwomba msaada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeteswa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana yeye hapuuzi au kudharau unyonge wa mnyonge; wala hajifichi mbali naye, ila humsikia anapomwomba msaada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hapuuzi Wala kuchukizwa na mateso ya anayeteswa, Wala hamfichi uso wake, Bali humsikia akimlilia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana yeye hapuuzi au kudharau unyonge wa mnyonge; wala hajifichi mbali naye, ila humsikia anapomwomba msaada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hakuubeza unyonge wake mnyonge, wala moyo wake hakuuchafukia, wala hakuuficha uso wake, asimwone, ila alimsikia, alipomlilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Enyi munaomwabudu Yawe, mumusifu! Mumutukuze, enyi wazao wote wa Yakobo! Mumwogope Mungu, enyi wazao wote wa Israeli!