Psalms 22:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulimwengu wote utakumbuka na kumrudia Mwenyezi-Mungu; jamaa zote za mataifa zitamwabudu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia Mwenyezi Mungu, nazo jamaa zote za mataifa zitasujudu mbele zake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulimwengu wote utakumbuka na kumrudia Mwenyezi-Mungu; jamaa zote za mataifa zitamwabudu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia BWANA, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia bwana, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulimwengu wote utakumbuka na kumrudia Mwenyezi-Mungu; jamaa zote za mataifa zitamwabudu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo watavikumbuka na kumrudia Bwana mapeoni pote pa nchi; yatakutambikia na kukuangukia makabila yote ya wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamasikini watakula na kushiba; wanaomutafuta Yawe watamusifu. Mungu awajalie waishi milele!