Psalms 27:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami kwa fahari nitaangalia juu ya maadui zangu wanaonizunguka. Nitamtolea tambiko kwa shangwe hekaluni mwake, nitaimba na kumshangilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami kwa fahari nitaangalia juu ya maadui zangu wanaonizunguka. Nitamtolea tambiko kwa shangwe hekaluni mwake, nitaimba na kumshangilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka; katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia BWANA na kumsifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia bwana na kumsifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami kwa fahari nitaangalia juu ya maadui zangu wanaonizunguka. Nitamtolea tambiko kwa shangwe hekaluni mwake, nitaimba na kumshangilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo sasa kichwa changu kitakuwa kimeinuka, kiwashinde wachukivu wangu wanizungukao; napo penye hema lake ndipo, nitakapomtambikia na kumtolea vipaji vya tambiko vya kumshangilia, nimchezee Bwana ngoma na kumwimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nitawaangalia kwa majivuno waadui zangu wanaonizunguka. Nitamutolea Yawe sadaka kwa shangwe, ndani ya hekalu lake, nitaimba na kumushangilia.