Psalms 28:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Zaburi ya Daudi) Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninakuita wewe, Ee Mwenyezi Mungu, Mwamba wangu; usikatae kunisikiliza. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, nitakuita Wewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Zaburi Ya Daudi) Ninakuita wewe, Ee BWANA, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na hao waliokwisha shuka shimoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninakuita wewe, Ee bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Bwana ninakuita, u mwamba wangu, usininyamazie na kuwa kimya, nisije kufanana nao washukao kuzimuni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, nitakuita Wewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaburi ya Daudi. Ninakulilia, ee Yawe! Ewe kikingio changu, usikuwe kama kiziwi kwangu. Usikuwe kama haunisikilizi, nisikuwe kama wale wanaoshuka katika shimo la wafu.