Psalms 29:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule, hukwanyua majani ya miti msituni, na hekaluni mwake wote wasema: “Utukufu kwa Mungu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauti ya Mwenyezi Mungu huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule, hukwanyua majani ya miti msituni, na hekaluni mwake wote wasema: “Utukufu kwa Mungu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauti ya BWANA huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauti ya bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauti ya BWANA yawazalisha ayala, Na kuiacha misitu wazi; Na ndani ya hekalu lake Wanasema, Utukufu!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule, hukwanyua majani ya miti msituni, na hekaluni mwake wote wasema: “Utukufu kwa Mungu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauti ya Bwana huzalisha kulungu, hutikisa miti ya mwituni, matawi yavunjike; kwa hiyo wote waliomo Jumbani mwake humtukuza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauti ya BWANA yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sauti ya Yawe inatikisa mivule, inaongoa majani ya miti ya pori, na wote wanaokuwa katika hekalu lake wanasema: “Utukufu kwa Mungu!”