Psalms 30:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini furaha huja asubuhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote; inawezekana kilio kikawepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani makali yake hukaa punde kidogo tu, kuwapa watu uzima ndiko kunakompendeza. Kama jioni tunakwenda kulala wenye kilio, asubuhi kimegeuka kuwa kicheko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumwimbie Yawe sifa, enyi waaminifu wake; mukumbuke utakatifu wake na kumushukuru.