Psalms 31:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maisha yangu yamekwisha kwa majonzi; naam, miaka yangu kwa kulalamika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maisha yangu yamekwisha kwa majonzi; naam, miaka yangu kwa kulalamika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maisha yangu yamekwisha kwa majonzi; naam, miaka yangu kwa kulalamika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani siku zangu zimeishia kwa masikitiko, miaka yangu nayo kwa kupiga kite, nguvu yangu imepondeka kwa manza, nilizozikora, hata mifupa yangu haina kiini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unionee huruma, ee Yawe, niko katika taabu; macho yangu yamechoka kwa ajili ya huzuni, nimeishiwa nguvu katika mwili na roho.